Thursday, July 19, 2012

MV Skagit, boti lililouzwa likiwa na hitilafu!!!!

Boti za MV Skagit na MV Kalama kabla ya kuuzwa na mamlaka ya bandari ya Washington.Boti hizo ziliuzwa baada ya kuchoka na kukosa fedha za kufanya restoration mnamo mwaka 2011.

boti ya MV Skagit kabla ya kuuzwa Zanzibar mwaka 2011.

Monday, July 16, 2012

WIZKID ADATA NA UBALOZI WA PEPSI.......!

Tha new kid on tha block, all tha way kutoka Naija, Wizkid ameonekana kudata baada ya kupewa ubalozi wa Pepsi. Chanzo kinachoaminika na kilichokaribu na familia hiyo kiliutonya mtandao mmoja nchini Naija kuwa jamaa amekuwa akijiona kama ndo Stardom inaisha kesho. kila heri Wizkid!

MAGAZETI YA LEO..............!


GOLDIE atolewa Big Bother Stargame!

baada ya kupeta ndani ya mjengo kwa siku 68, mwanamuziki kutoka Nigeria, Goldie atolewa ndani ya Big Brother Stargame.
Mwanadafada huyo mwenye umri wa miaka 28, alitolewa jana jumapili, wakati wa kipindi cha mtoano. Alipigiwa kura 15 za kutolewa, akifuatiwa na Lady May aliyepata 3, na Prezzo aliyepata 6.
Kabala ya kuanza kipindi Goldie alijitabiria kutoka mapema na alimwaqmbia Big, maneno haya:
"ningependa iwe tofauti. siwezi kufanya iwe hivyo. naomba iwezekane, lakini kwa sababu fulani, najua haitkuwa tofauti"

Saturday, July 14, 2012

J.LO AKACHA AMERICAN IDOL

Mwanamuziki na muigizaji mkongwe all tha way kutoka kwa Obamaland, Jennifer Lopez, ameikacha American Idol. The Inside Source bila wasiwasi zimeinyaka nyuzi kuwa the super n' famous judge huyo ametimka kwa sababu zake binafsi, ila AMERICAN IDOL iko mezani na mazungumzo ili kumshawishi Mariah Carey kuziba pengo la mwanamama huyo.

BEANIE SIGEL ANATARAJIA KUZINDUA ALBAMU KABLA YA KWENDA JELA

Msanii ambaye alikutwa nakosa la tax evasion, Beanie Sigel anatarajia kuzindua albamu yake ya tano iitwayo THIS TIME. Sigel amepanga kuzindua albamu yake tarehe 28 september kabla ya kuanza kifungo cha miaka miwili mnamo tarehe 12 septemba.

MTOTO WA SYLVESTER STALLONE AAGA DUNIA!

Mtoto wa kiume wa muigizaji mkongwe nchini Marekani, Sage Stallone,36 amekutwa amekufa katika apartment moja huko Hollywood. Sage ambaye alionekana kwenye film kwa mara ya kwanza akiwa na baba yake katika filamu ya Rocky V, akicheza kama mtoto wa Rocky Balboa.
Kifo hicho kimethibitishwa na mwanasheria wake, na imesemekana kuwa ilibidi afunge arusi hivi karibuni. Vyanzo mbalimbali vimesema kifo hicho kilitokana kuzidisha dawa, pill taking overdose.

Wednesday, July 11, 2012

UMAARUFU NI NYOTA, HATA UZEENI HUJA!!!!

Leo tunacheki watu watatu waliopata umaarufu wasioutegemea na katika nyakati tofaouti. wafuatao ni watu waliopata umaarufu pasipo kutegemea wakati umri ukielekea kuwatupa mkono
1. Babu wa Loliondo
   mzee ambaye inaaminika kuwa alianza kazi ya kuwaponya watu kwa kutumia miti shamba baada ya kuacha uchungaji , hivyo kujizolea umaarufu kwenye nchi ya Jakaya, 255 area code. jina lake kamili ni Ambilikile Mwasapila.

2. Bibi Cheka
bibi ambaye alianza kama utani kwa kuhojiwa tu kwa media akiwa na umri wa miaka 50, lakini baadaye anarock na kutetemesha in area coded 255. kwa sasa bi Cheka yupo na Mkubwa na Wanawe na anahit  na track yake kwa hewa dubbed 'ni wewe'.

Tuesday, July 10, 2012

HASHEEM THABEET na new big deal with Thunder!

jembe linalofanya pouwa kunako anga la mpira wa kikapu nchini Marekani - NBA league, Hasheem Thabeet, amejiunga na wakali kutoka Western Conference, Oklahoma City Thunder kwa mkataba wa miaka miwili.
The big tall man huyo ambaye alishika nafasi ya pili kutokana na draft iliyofanya na Memphis Grizzlies. Teams alizopiga mzigo ni HOUSTON na PORTLAND.
Wakala wa mchezaji huyo, Bill Duffy, amethibitisha kufanyika kwa kuchukuliwa kwa big man huyo ambaye atajiunga na THUNDER ili kumsaidia center Kendrick Perkins, ingawa anategemea kupata upinzani kutoka kwa Cole Andrich. kila la heri the big man 7-FOOT-3 Center!!!!!!

DIVA naye kwa mikogo, kuolewa dili enhe!

mwanadada anayetamba na sauti yake kunako Clouds FM's Ala za Roho, Loveness Love Malinzi a.k.a Diva jana alifunguka kwenye XXL wakati wa Hot 3 na Adam Mchomu kuwa atakayemuoa lazima awe na mahari si chini ya millioni 500. je, siku hizi kuolewa ni asset?

FIDSTYLE FRIDAY ndani ya EATVKutoka ndani ya kiwanda cha burudani Bongo, CheusiDawa Entertainment, as owned na icon anyefanya poa kwenye game la muziki, Fareed "Fid Q" Kubanda, itarajia kuachia kipindi chake cha FIDSTYLE FRIDAY, na hii ni baada ya kupeta kwenye stream ya youtube na mtandao wake binafsi, www.cheusidawa.tv.
                                                                                                        Cha kufanya ni kukaa karibu na ting'a
                                                                                                         namba moja kwa vijana, EATV.

RVP akana kurenew mkataba wake na Arsenal

Mwenyekiti wa zamani wa Arsenal, David Dein amesema anatarajia kuwa mshambuliaji hatari kutoka Uholanzi, Robin Van Persie, anaweza akaondoka klabuni hivi punde ingawa Arsenal inatarajia kufanya juu chini ili kumbakiza klabuni.
RVP amebakiwa na mkataba wa mwaka mmoja na washika mtutu hao wa London, ingawa kuna tetesi kuwa huenda mholanzi huyo anaweza akajiunga na wabishi wa Serie A, Juventus na mabingwa wa EPL, Manchester City kwa kipindi cha majira ya joto.
RVP aliandika hayo katika mtandao wake binafsi na alisema anapenda kuwa na furaha wakati wote ila kwenye klabu itakayompa raha maishani.