Monday, June 24, 2013

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA MATHIAS KISSA

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2013/06/Tenga-wa-TFF1.jpg 
Na Boniface Wambura
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mchezaji wa zamani wa timu za Cosmopolitan na Taifa Stars, Mathias Kissa (84) kilichotokea leo alfajiri (Juni 24 mwaka huu) kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
 Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani enzi zake, Kissa akiwa na timu ya Tabora alitamba katika michuano ya Kombe la Taifa wakati huo ikiitwa Sunlight Cup. Alikuwa akicheza katika nafasi ya ulinzi.
 Baadaye alijiunga na Cosmoplitan ya Dar es Salaam, na pia kuwa mchezaji wa timu ya Taifa ambapo enzi zake akiwa na wachezaji kama Yunge Mwanansali wakiiwakilisha Tanganyika na baadaye Tanzania Bara walitamba katika michuano ya Kombe la Chalenji wakati huo ikiitwa Gossage, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
 Kissa ambaye alipata tuzo ya mchezaji bora wa karne kwa upande wa Tanzania, tuzo inayotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) alikuwa ndiye mchezaji msomi kupita wote wakati akichezea timu ya Taifa akiwa amehitimu elimu ya Darasa la Kumi.
 Kwa mujibu wa binti yake, Erica, marehemu ambaye pia aliwahi kuwa mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi (stroke) alioupata miaka mitano iliyopita, na kisukari. Baadaye alipata kidonda ambacho ndicho kilichosababisha kifo chake.
Msiba uko nyumbani kwa marahemu, Masaki, Mtaa wa Ruvu karibu na Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST). Maziko yatafanyika keshokutwa, Jumatano (Juni 26 mwaka huu) kwenye makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
 TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Kisa, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na klabu ya Cosmopolitan na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Mungu aiweke roho ya marehemu Kisa mahali pema peponi. Amina

PICHA ZA WAZIRI MKUU MHE. PINDA AKIFUNGUA MKUTANO WA MADC, MARC NA MARAS NA BUNGENI MJINI DODOMA

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2013/06/IMG_0030.jpgBaadhi ya Wakuu wa Mikoa wakinukuu maelekezo ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipofungua  Mafunzo  ya Kujenga Uwezo kwa Wakuu wa Wilaya , Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Mikoa kwenye ukumbi wa Hoteli ya New Dodoma mjini Dodoma  Juni 24,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2013/06/IMG_0037.jpg 
Baadhi ya Wakuu wa  Wilaya wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipofungua  Mafunzo  ya Kujenga Uwezo kwa Wakuu wa Wilaya , Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Mikoa kwenye ukumbi wa Hoteli ya New Dodoma mjini Dodoma  Juni 24,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  
IMG_0050
Waziri Mkuu MizengoPinda akihutubia wakati alipofungua  Mafunzo  ya Kujenga Uwezo kwa Wakuu wa Wilaya , Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Mikoa kwenye ukumbi wa Hoteli ya New Dodoma mjini Dodoma  Juni 24,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)IMG_0143

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na wabunge, Bungeni Mjini Dodoma 24,2013.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na wabunge, Bungeni Mjini Dodoma 24,2013.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na wabunge, Bungeni Mjini Dodoma 24,2013.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na wabunge, Bungeni Mjini Dodoma 24,2013.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)IMG_0161

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na wabunge, Bungeni Mjini Dodoma 24,2013.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Friday, June 21, 2013

MADAWA YA KULEVYA NI NOUMER!!!

jana kwenye bonge la talk show hapa town, THE MBONI TALK SHOW, ishu ilikuwa ni kuhusu madawa ya kulevya . kilichonishangaza ni kuona vijana wazuri nao pia walijiingiza kwenye madawa ya kulevya.
EPUKA MADAWA YA KULEVYA, CHAGUA MAISHA!!!

Mbunge wa kasulu mjini kupitia tiketi ya Chama cha NCCR Mh. Moses Machalli

Habari zilizoifikia Maisha Times muda huu kutoka Dodoma zinaripoti kwamba Mbunge wa Kasulu mjini kupitia tiketi ya Chama cha NCCR Mh. Moses Machalli amevamiwa na kupigwa na watu wasiojulikana katika eneo la, tukio hilo limetokea jioni hii wakati Mh. Machalli akiendesha gari lake mita kadhaa kutoka ilipo nyumba anayoishi baada ya kuwapigia honi vijana kadhaa waliokuwa wakitembea katikati ya barabara ili wasogee pembeni naye aweze kupita kitendo ambacho kilionekana kuwaudhi na kuwakera vijana hao ambao walianza kuipiga na kuigonga kwa nguvu bodi ya gari ya Mh. Machalli jambo ambalo lilimfanya Machalli kusimamisha gari na kushuka ili kujua kulikoni hali iliyopelekea vijana hao kumtolea matusi kadhaa ya nguoni na pindi machalli alipowajibu kwa hasira ndipo kipigo kikali kilipoanzia.

Shuhuda wetu aliyekuwa jirani na eneo la tukio anasema kwamba Mh. Machalli amepigwa na vijana zaidi ya nane jambo ambalo lilipelekea hata yeye kushindwa kumsaidia kwa kuhofia kuunganishwa katika kipigo.

Maisha Times itazidi kukuhabarisha zaidi kuhusiana na tukio hili kadiri habari zitakavyozidi kupatikana.

Thursday, June 20, 2013

NEW JOINT!!!!

Stoppa The Rhymecca feat Joh Makini

HII INAKUHUSU!!!!


PICHA MBALIMBALI ZA UTENGENEZAJI WA VIDEO MPYA YA IZZO BIZNESS, LOVE ME!

Mbeya City Native, Emmanuel Simwinga, known by his stage name Izzo Bizness alikuwa akishoot video mpya ya wimbo wake wa LOVE ME. Video imefanywa na Nick Dizzo wa E-Media , na hizi ni picha wakati wa tukio hilo: