Thursday, October 10, 2013

Dk. Slaa atembelea NASA, aionya CCM kuhusu fursa za sayansi nchini   
Dr. Slaa akiangalia kwa umakini Apollo 16 capsule kwa umakini. Hii ni Capsule iliyorudi kutoka mwezini miaka ya 70

    Katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Dr. Wilbrod Slaa leo amezuru Shirika la Anga la Marekani Nasa huko Huntsville ambako alilakiwa na mkurugenzi mkuu wa shirika hilo. Dr. Slaa alifika hapo kujifunza mambo mbali mbali ikiwemo namna ya kuwashirikisha na pia kuwapa vijana wa kitanzania changamoto ili waweke jitihada zaidi kwenye masomo ya sayansi ili kuinyanyua Tanzania kutoka kwenye shimo la umasikini.
        Dr. Slaa amesema kwamba, hadi kufika marekani, wanasayansi wa kimarekani walifika mwezini baada ya kupata changamoto kutoka kwa Rais keneddy aliyewamba wanasayansi hao kufikisha mtu mwezini chini ya miaka 10. Wanasayansi hao walimjibu na kufika mwezini chini ya miaka 8. Hii ilitokana na serikali ya marekani kuipa kipaumbele elimu
        Dr. Slaa aliendelea kusema kwamba baada ya uhuru, Mwalimu Nyerere aliipa kipaumbele elimu kwa ujumla. Kwa mfano, Mwalimu Nyerere aliwachukua vijana watano wanajeshi na kuwapeleka nchini Ireland kusomea mambo ya engineering. Waliporudi walipelekwa kibaha ambako walibuni na kutengeneza gari ya kwanza iliyoitwa Nyumbu ambayo ni ubunifu wao.

         Baadae mwalimu Nyerere aliwabunia hao wanajeshi mradi wa Dhaabu wa Buhemba ambao ungewawezesha kulipia gharama za kutengeneza magari mengi. Bahati mbaya, baada ya mwalimu kustaafu, mafisadi walijipenyeza na kuuchukua huo mradi. Huu ndio ufisadi uliozaa meremeta. Mradi wa Nyumbu ukafa na kilichotokea ni ufisadi wa billion 155 uliohusisha benki ya Nedeland Ya Afrika kusini. Hadi leo, hakuna maelezo licha ya fedha hizo kutumika kwenye kampeni ya CCM ya 1995
      CCM imekuwa janga la mtanzania. CCM inaua ubunifu wa vijana wetu. Leo 90% ya wanafunzi wanafeli mashuleni huku viongozi wa CCM wakiwahadaa wananchi kwamba wanaleta maendeleo. Ni maendeleo gani wanazungumzia wakati watoto wetu hawajui kusoma wala kuandika alihoji Dr. Slaa. Wanajeshi wetu waadilifu, wabunifu, wazalendo na wanaojituma wamefikia kuishi maisha ya ajabu.
        Ubunifu wao kama mradi wa Nyumbu umeuwawa na CCM. CCM imefanya maisha yao kuwa magumu naya kusikitisha. Wanajeshi waliostaafu wamebaki kama omba omba. Wale wanashiriki kulinda amani nje ya nchi wanadhulumiwa hela zao pale wanarudi Tanzania. Nchi ambayo haiwezi kuwahudhumia wanajeshi wake, ni nchi isiyofaa kuwa katika ramani ya dunia. Dr. Slaa amewaomba wanajeshi wasilie, kwani CHADEMA inatambua michango yao.
 
       Kadhalika amewaomba vijana watanzania wasikate tamaa. CHADEMA inasikia vilio vyao, wanatambua kwamba ugumu wao wa maisha umesababishwa na CCM na siyo mwingine. Wakati hao ma CCM wanajineemesha na hela zetu za kodi, wanajeshi na wananchi kwa ujumla wanashindwa hata kujenga nyumba ya kujisitiri punde wanapostaafu. CCM imeua ubunifu ndani ya Tanzania. Wameamua kuwaweka vijana wetu mazezeta ili waendelee kuwatawala. Wenzetu wanapeleka watu mwezini, lakini watanzania hata wembe tunanunua kutoka chini kwa sababu ya CCM alisema Dr. Slaa na kuonya kwamba wakiendelea kuwanyima wananchi haki zao za msingi, muda utafika watachoka

Rover Ambayo imewahi kutumika mwezini


Dr. Slaa akipokea zawadi maalum ambayo rais wa marekani tu ndiye aliyewahi kupewa