Tuesday, July 10, 2012

RVP akana kurenew mkataba wake na Arsenal

Mwenyekiti wa zamani wa Arsenal, David Dein amesema anatarajia kuwa mshambuliaji hatari kutoka Uholanzi, Robin Van Persie, anaweza akaondoka klabuni hivi punde ingawa Arsenal inatarajia kufanya juu chini ili kumbakiza klabuni.
RVP amebakiwa na mkataba wa mwaka mmoja na washika mtutu hao wa London, ingawa kuna tetesi kuwa huenda mholanzi huyo anaweza akajiunga na wabishi wa Serie A, Juventus na mabingwa wa EPL, Manchester City kwa kipindi cha majira ya joto.
RVP aliandika hayo katika mtandao wake binafsi na alisema anapenda kuwa na furaha wakati wote ila kwenye klabu itakayompa raha maishani.

No comments:

Post a Comment